Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Padri huyo alissilimu hivi karibuni na kuwafanya waumini wake wote kujiunga na imani ya ukweli ya kiislamu.
Tukio hilo limetokea siku ya Jumanne tarehe 25 mwezi wa nane mwaka huu ambapo Padri huyo alikusanyika na waumini wake wapatao 480 kwaajili ya ibada, lakini baada ya kuwaeleza kuwa kwake mwisilamu, waumini wake pia waliamua kuwa waislamu na kupata sharafu ya uislamu.
Padri huyo ambaye ni mwananchi wa Rwanda alifanya mazungumzo marefu na mwanazuoni mmoja wa kiislamu nchini humo mpaka kufikia hatua ya kukiri kuwa uislamu ndio dini ya haki, kitu ambacho kilipelekea waumini wake nao kukinai na ukweli wa dini ya kiislamu na kufuata ukweli alioukubali kiongozi wao, huku wakilifanya kanisa hilo kuwa msikiti.